MWAMBIENI FEITOTO

 Mwambieni FEI TOTO KUWA:- 




1. Kiwango chake na cha Pacome havitofautiani sana. Aongeze bidii kidogo tu atamkuta na Kumpita.

2. ⁠Mkumbusheni Fei Kuwa kuna club kubwa mbili tu hapa Nchini, Simba na Yanga. Akitaka kuonekana ukubwa wake lazima acheze moja ya club hizi.

3. ⁠Mwambieni kadri mashabiki wanavyokuimba vizuri huku nje humwongezea Mchezaji kujiamini na kufuatiliwa kwa ukaribu na club nyingine. Hii ndio faida kubwa toka kwa mashabiki kwenda kwa mchezaji.

4. ⁠Kwambieni Fan Base inayoweza kumuuza Fei Toto nje ya Mipaka ya Tanzania ni aidha ya Yanga au ya Simba. 

5. ⁠Fan Base ya Yanga kashatibuana nayo siku akifanikiwa kupiga Press awaombe Msamaha hakuna atakachopungukiwa ili wasiendelee kumtumkana hii inampunguzia Mchezaji kujiamini.

6. ⁠Mwambieni pale Simba kuna Fursa imejitokeza. Kiungo wao mpendwa Chama Wamemsimamisha, najua wapo Sokoni kutafuta Mbadala. Aongee na wakala wake aende Pale Simba awaombe wakaongee na Azam wavunje mkataba wake ahamie Simba chap, kuna faida nyingi atazipata hata kama mshahara wake hautofikia anaolipwa na wana lambalamba.

7. ⁠Ni rahisi kwa sasa kumuuza Mudathiri nje ya Nchi kuliko Feisal. Achukulie mfano huu nani alimuimba Mudathiri kabla ya kuhamia Yanga? 

8. ⁠Manula, Erasto Nyoni, Kapombe, Bocco na wengineo walicheza misimu kadhaa Pale Azam lakini maisha yao ya Soka yalibadilishwa sana walipohamia Simba. Au nani anamkumbuka Bangala na Djuma Shaban?

9. Umri wake unaruhusu bado sana kufanya vitu vingi uwanjani.

10. Hapa nchini kuna wachezaji wazuri sana kwenye timu nyingine lakini usipocheza kwa kurwa na Dotto wa Kariakoo utastaafu ukiwa hujulikani popote.


Comments

Popular posts from this blog

JAMAA AREKODI VIDEO AKIFANYA MAPENZI NA WANAWAKE 400 TOFAUTI

MUIGIZAJI GRACE MAPUNDA AFARIKI DUNIA